Eng. Peter Ulanga

CEO & Fund Manager: UCSAF

Girls in ICT Day - Tanzania

Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) imeandaa warsha ya uvumbuzi wa teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa wasichana wadogo wa shule za sekondari nchini kote. Warsha hii inalenga katika kuleta msukumo kwa wasichana wa Tanzania kujihusisha na TEHAMA katika kufanikisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya jamii zao na pia kuandaa mabalozi watakaoiwakilisha Tanzania kwenye siku ya Watoto wa kike na TEHAMA inayotarajiwa kuadhimishwa baadae mwezi huu huko Addis Ababa nchini Ethiopia. Siku hii ya Watoto wa kike na TEHAMA ni jitihada za ITU katika kuongeza uelewa juu ya kuwawezesha na kuhamasisha wasichana na wanawake vijana kufikiria masomo na kazi katika teknolojia ya Habari na Mawasiliano. Siku hii huudhamishwa kila mwaka kwenye nchi mbali mbali duniani ambao ni wanachama wa umoja huo, Tanzania ikiwemo.

Kwa wiki mbili mfululizo Mfuko umewahusisha wasichana 240 wa shule za sekondari nchini kote katika mafunzo ya TEHAMA kwa kuwapatia stadi muhimu kupitia njia kuu tatu ambazo ni uvumbuzi, ujuzi na uzoefu. Warsha hii na mafunzo imefanyika katika jumla ya kanda sita (6) ambayo ni pamoja na Kanda ya Ziwa (Mwanza), Kanda ya Kati (Dodoma), Kanda ya Kaskazini (Arusha), Nyanda za Juu Kusini (Mbeya), Zanzibar (Unguja) na Kanda ya Mashariki (Dar es Salaam). Katika ngazi ya Taifa, wanafunzi thelathini (30) watashindana na kati yao wanafunzi sita bora (6) wataiwakilisha Tanzania katika siku ya kimataifa ya mtoto wa kike na TEHAMA itakayoadhimishwa Alhamisi ya Aprili 28, 2016 mjini Addis Ababa Ethiopia. 

Girls in ICT 2016

Pia katika warsha hii wanafunzi watapata fursa ya kukutana na wanawake na akina mama ambao wamefanikiwa katika nyanja mbalimbali hasa katika teknolojia ya habari na mawasiliano na pia wafanyabiashara wakubwa na viongozi wa taasisi za kiserikali na kimataifa kwa ajili ya kuwatia hamasa katika kutimiza ndoto zao.

Girls in ICT 2016

Fungua Picha Zaidi ...

Habari na Matukio
Ziara ya Kamati ya Miundombinu
Tarehe : 2018-07-11

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imefanya ziara katika ofisi za Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwa ajil ...

Zaidi
UTEUZI WA MWENYEKITI WA BODI YA MFUKO WA MAWASILIANO KWA WOTE
Tarehe : 2016-09-07

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi an Mawasiliano Mheshimiwa Prof. Makame Mbarawa (Mb) kwa mamlaka aliyonayo chini ya kifungu ...

Zaidi
Girls in ICT Day - Tanzania
Tarehe : 2016-04-06

Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) imeandaa warsha ya uvumbuzi wa teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa ...

Zaidi