Eng. Peter Ulanga

CEO & Fund Manager: UCSAF

Ziara ya Kamati ya Miundombinu

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imefanya ziara katika ofisi za Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwa ajili ya kukagua shughuli za Mfuko. Ziara hiyo imefanyika tarehe 11 Julai, 2018. Kamati hiyo ilikutana  na Bodi pamoja na Menejimenti ya Mfuko. Katika ziara hiyo, Kamati iliongozwa na Mwenyekiti Mhe. Moshi Seleman Kakoso, akisaidiwa na Makamu Mwenyekiti Mhe. Hawa Mchafu Chakoma. Aidha, kamati iliongozana na Menejiment ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wakiongozwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Atashasta Nditiye (Mb) akiambatana na Eng. Angelina Madete, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano).

Baada ya ufunguzi wa kikao hicho, Mtendaji Mkuu wa Mfuko Eng. Peter Ulanga alitoa wasilisho kuhusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo zifanywazo na Mfuko ikiwemo miradi ya kufikisha huduma ya mawasiliano vijijini, kuunganisha mashule na mtandao wa intaneti, kutoa mafunzo ya TEHAMA kwa Walimu wa shule za msingi na sekondari. Miradi mingine inayotekelezwa na Mfuko ni pamoja na tiba mtandao, mawasiliano ya kidigitali ya runinga pamoja na ujenzi wa vituo vya TEHAMA.

Mpaka sasa, jumla ya kata 530 zenye jumla ya vijiji 2,132 pamoja na wakazi zaidi ya milioni 3.6 zimekwisha ainishwa kufikishiwa huduma za mawasiliano kupitia ruzuku ya serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote. Kata 468 kati ya kata 530 zenye vijiji 1,980 na zaidi ya wananchi milioni 3.2 zimekwisha pata huduma ya mawasiliano ambayo ni sawa na asilimia 88 ya miradi hiyo. Ruzuku ya fedha za kitanzania bilioni 95.7 zimetumika kukamilisha miradi hiyo.

Baada ya wasilisho hilo, Kamati ya Bunge ilipata wasaa wa kujadili taarifa ya Mfuko na kuuliza maswali mbalimbali yaliyojibiwa na Mtendaji Mkuu wa Mfuko. Aidha, Mhe. Nditiye alitoa ufafanuzi kuhusu masuala ya kisera, na kuwaahidi waheshimiwa wabunge kuwa Serikali itaendelea na adhima yake ya kufikisha huduma ya mawasiliano vijijini ili hatimaye wanananchi wengi wapate huduma hiyo.

Katika majumuisho ya kikao, Mwenyekiti wa kikao, alimpongeza Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko, Dr. Joseph Kilongola, pamoja na Bodi nzima na Menejiment kwa kazi nzuri ya kufikisha huduma za mawasiliano vijijini. Aidha, alisisitiza umuhimu wa kuwasimamia watoa huduma wote wakamilishe utekelezaji wa miradi kwa mujibu wa mikataba na kwa wakati uliokubaliwa.

Habari na Matukio
Ziara ya Kamati ya Miundombinu
Tarehe : 2018-07-11

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imefanya ziara katika ofisi za Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwa ajil ...

Zaidi
UTEUZI WA MWENYEKITI WA BODI YA MFUKO WA MAWASILIANO KWA WOTE
Tarehe : 2016-09-07

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi an Mawasiliano Mheshimiwa Prof. Makame Mbarawa (Mb) kwa mamlaka aliyonayo chini ya kifungu ...

Zaidi
Girls in ICT Day - Tanzania
Tarehe : 2016-04-06

Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) imeandaa warsha ya uvumbuzi wa teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa ...

Zaidi