Waziri Nnauye apongeza ujenzi wa minara ya UCSAF, Zanzibar

  • 20 May, 2022
Waziri Nnauye apongeza ujenzi wa minara ya UCSAF, Zanzibar

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amefanya ziara ya kikazi katika visiwa za Unguja na Pemba kukagua ujenzi wa minara ya mawasiliano ya simu ambayo inajengwa na kampuni ya mawasiliano ya Zanzibar(Zantel) kwa ruzuku inayotolewa na Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF).

Mwezi Januari 2022, UCSAF na Zantel waliingia makubaliano ya kujenga minara 42 ya mawasiliano ya simu katika shehia (kata)38 vsiwani humo kwa ruzuku ya jumla ya shilingi Bilioni sita, milioni mia tisa na mbili na laki saba. Hadi sasa ujenzi wa minara takribani 37 umekamilika na michache iliyosalia inatarajiwa kukamilika mwezi Juni 2022.

Katika utekelezaji wa mradi huo, zantel inatakiwa kujenga minara yenye uwezo wa kutoa huduma ya sauti (teknolojia ya 2G) pamoja na huduma ya mtandao wa intaneti inayowezeshwa na teknolijia ya 3G. Pia minara hiyo itakuwa na uwezo wa kuruhusu watoa huduma  wengine wa mawasiliano ya simu, watoa huduma wengine wa TEHAMA kama vile watoa huduma za intaneti (Traditional ISP), Redio na runinga kutumia mnara huo kutoa huduma.

Waziri Nnauye ameipongeza UCSAF na Zantel kwa kusimamia na kuhakikisha kuwa mradio huo wa kimkakati unakamilika ndani ya muda mfupi ili kuwawezesha wananchi kuanza kupata huduma ya mawasiliano katika maeneo ambayo minara hiyo inajengwa.

Mradi huu utakapokamilika utatatua changamoto ya mawasiliano kwa wananchi wapatao 209,904 kutoka katika Shehia (Kata) 38 zenye vijiji 78.