Eng. Peter Ulanga

CEO & Fund Manager: UCSAF

Kuhusu UCSAF

Malengo ya Mfuko
Kazi za Mfuko
Muundo wa Mfuko
Wajumbe wa Bodi

Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (Mfuko) ulianzishwa na Serikali kwa sheria namba 11 ya mwaka 2006 ambayo ilipewa jukumu kuu la kupeleka mawasiliano vijijini. Mwaka 2009 kanuni za kuhuisha Mfuko zilipitishwa na ni katika kipindi hicho ambapo Mtendaji Mkuu wa Mfuko pia aliteuliwa kwa mujibu wa sheria.

Mchakato wa ajira ya watendaji wengine ilichukua muda mrefu kukamilika hadi mwezi Septemba 2012 ambapo watendaji wengine walianza kuajiriwa na utekelezaji wa majukumu ya Mfuko ukaendelea.


MALENGO YA MFUKO

Malengo ya Mfuko kama yalivyoainishwa na sheria ni haya yafuatayo:-

 1. Kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya mawasiliano katika maeneo ya vijijini na maeneo ya mijini yenye mawasiliano hafifu;
 2. Kuhamasisha ushiriki wa sekta binafsi na serikali katika utoaji wa huduma za mawasiliano kwa wote katika maeneo ya vijijini na maeneo ya mijini yenye mawasiliano hafifu;
 1. Kuhamasisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika maeneo ya vijijini na maeneo ya mijini yenye mawasiliano hafifu;
 1. Kutengeneza mfumo kwa ajili ya upatikanaji wa mitandao ya mawasiliano na huduma rahisi na zenye ufanisi katika uzalishaji na upatikanaji katika soko la kiushindani;
 1. Kuhamasisha utoaji wa huduma bora katika viwango nafuu na kuhakikisha kuwa teknolojia ya habari na mawasilianpo inapatikana vijijini na sehemu za mijini zenye mawasiliano hafifu kwa bei nafuu; na
 2. Kuhakikisha upatikanaji wa huduma za wote kwa kuboresha upatikanaji wa huduma za mawasiliano kupitia ushiriki wa sekta binafsi.

KAZI ZA MFUKO

Majukumu ya Mfuko kama yalivyoainishwa na sheria ni haya yafuatayo:-

 1. Kubainisha maeneo ya miradi ya mawasiliano ambayo yanaweza kupata ruzuku kutoka katika Mfuko;
 2. Kuweka vigezo vya utambuzi wa maeneo ya vijiji vinavyohitaji na ambavyo haviwezi kupata huduma ya mawasiliano kwa sababu havina mvuto wa kibiashara;
 3. Kuanzisha mfumo madhubuti wa usimamizi wa fedha;
 4. Kuweka vigezo sahihi vya utoaji wa ruzuku kwa watoa huduma za Mawasiliano kwa ajili ya kupeleka mawasiliano katika maeneo yaliyoainishwa;
 5. Kufanya tafiti mbalimbali na kufuatilia maendeleo ya mawasiliano katika maeneo ya vijijini na yale yasiyo na mvuto wa kibiashara;
 6. Kuishauri Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuhusiana na mambo yanayohusu Mawasiliano kwa wote;
 7. Kuangalia njia sahihi za kutoa ruzuku kwa ajili ya kupeleka huduma ya mawasiliano vijijini na katika maeneo yasiyo na mvuto kibiashara;
 8. Kusimamia kisheria mikataba ya utekelezaji wa majukumu ya utoaji wa huduma za mawasiliano kwa wote;
 9. Kuendesha na Kuendeleza Mfuko kama  ulivyoanzishwa;
 10. Kuweka utaratibu mzuri wa kusimamia, kukokotoa na kukusanya tozo za Mawasiliano kwa wote kutoka kwa watoa huduma;
 11. Kukokotoa, kupanga na kugawanya ruzuku za mawasiliano kwa wote;
 12. Kupendekeza sera madhubuti za Mfuko kwa Waziri wa Sekta ya Mawasiliano;
 13. Kusimamia rasilimali fedha za Mfuko na kuhakikisha matumizi yanayofanywa na Mfuko yanakuwa yenye manufaa kwa jamii;
 14. Kushauriana na Kushirikiana na Wizara za Serikali, Idara au Mamlaka inayojitegemea kuhusiana na masuala ya huduma kwa wote; na
 15. Kutengeneza Miongozo mbalimbali kwa ajili ya uendeshaji wa Mfuko.

Rudi mwanzo ↑


Muundo wa Mfuko

Rudi mwanzo ↑


Wajumbe wa bodi

Mwenyekiti wa Bodi                     

Dkt. Joseph S. Kilongola

Mwenyekiti 

 

Mr. Godfrey SimbeyeMr. Godfrey Simbeye

Mjumbe 

 

Eng. Peter Ulanga                     

Eng. Peter Ulanga

Mjumbe 

 

Eng. James KilabaEng. James M. Kilaba

Mjumbe 

 

                    

Mr. Lawrence Mworia

Mjumbe 

 

                     

Mr. Francis Mtete Chachah

Mjumbe 

 

                     

Ms. Eunice Masigati

Mjumbe 

 


Rudi mwanzo ↑

Misheni Yetu

Kuwezesha na kuratibu upatikanaji wa huduma za mawasiliano vijijini na na maeneo ya mijini yenye maendeleo duni kwa kushirikiana na wadau wengine wa  sekta ya mawasiliano ili kufikia maendeleo ya kiuchumi na kijamii sambamba na dira ya Maendeleo ya Tanzania ifikapo mwaka 2025

Uono wetu

Kufanikisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano Tanzania kikamilifu na kwa usawa

Habari na Matukio
Ziara ya Kamati ya Miundombinu
Tarehe : 2018-07-11

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imefanya ziara katika ofisi za Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwa ajil ...

Zaidi
UTEUZI WA MWENYEKITI WA BODI YA MFUKO WA MAWASILIANO KWA WOTE
Tarehe : 2016-09-07

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi an Mawasiliano Mheshimiwa Prof. Makame Mbarawa (Mb) kwa mamlaka aliyonayo chini ya kifungu ...

Zaidi
Girls in ICT Day - Tanzania
Tarehe : 2016-04-06

Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) imeandaa warsha ya uvumbuzi wa teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa ...

Zaidi