MIRADI YA MAWASILIANO VIJIJINI ILIYOKAMILIKA KWA KIPINDI CHA JULAI 2022 – JUNI, 2023

  • 26 August, 2023
MIRADI YA MAWASILIANO VIJIJINI ILIYOKAMILIKA KWA KIPINDI CHA JULAI 2022 – JUNI, 2023

Kwa kipindi cha kuanzia Julai 2022 mpaka Juni 2023, Jumla ya minara 304 imejengwa katika kata 291 zenye vijiji 580 ambapo jumla ya wananchi 3,343,565 wamenufaika na miradi hiyo. Watoa huduma watano wamekamilisha miradi yao kama ifuatavyo:-

  1. TTCL amewasha minara 72;
  2. VODACOM amewasha minara 17;
  3. AIRTEL amewasha minara 33;
  4. HALOTEL amewasha minara 123; na
  5. MIC amewasha Minara 59.

Aidha, UCSAF inaendelea na ukaguzi wa minara yote iliyowashwa kwa ajili ya kujiridhisha kuwa utendaji kazi wake unakidhi vigezo vilivyowekwa kwa mujibu wa mikataba.