- Kubaini maeneo ya miradi ya mawasiliano ambayo yanaweza kupata ruzuku kutoka katika Mfuko;
- Kuweka vigezo vya utambuzi wa maeneo ya vijiji vinavyohitaji na ambavyo haviwezi kupata huduma ya mawasiliano kwa sababu havina mvuto wa kibiashara;
- Kuweka vigezo sahihi vya utoaji wa ruzuku kwa watoa huduma za Mawasiliano kwa ajili ya kupeleka mawasiliano katika maeneo yaliyoainishwa;
- Kutathmini miradi ya mawasiliano inayowasilishwa na waatoa huduma ili kupewa ruzuku na Mfuko;
- Kufanya tafiti mbalimbali na kufuatilia maendeleo ya mawasiliano katika maeneo ya vijijini na yale yasiyo na mvuto wa kibiashara;
- Kuishauri Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuhusiana na mambo yanayohusu Mawasiliano kwa wote;
- Kuangalia njia sahihi za kutoa ruzuku kwa ajili ya kupeleka huduma ya mawasiliano vijijini na katika maeneo yasiyo na mvuto kibiashara;
- Kusimamia kisheria mikataba ya utekelezaji wa majukumu ya utoaji wa huduma za mawasiliano kwa wote;
- Kuweka utaratibu mzuri wa kusimamia, kukokotoa na kukusanya tozo za Mawasiliano kwa wote kutoka kwa watoa huduma;
- Kukokotoa, kupanga na kugawanya ruzuku za mawasiliano kwa wote;
- Kupendekeza sera madhubuti za Mfuko kwa Waziri wa Sekta ya Mawasiliano;
- Kushauriana na Kushirikiana na Wizara za Serikali, Idara au Mamlaka inayojitegemea kuhusiana na masuala ya huduma kwa wote.