UJENZI WA MINARA YA MAWASILIANO ZANZIBAR

  • 28 August, 2023
UJENZI WA MINARA YA MAWASILIANO ZANZIBAR

Ikiwa ni mwendelezo kwa kuboresha huduma za mawasiliano nchini, Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) umekamilisha ujenzi wa minara 42 iliyojengwa katika shehia(kata) 38 visiwani Zanzibar. Mradi huu ni kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kutangaza utalii.

Kukamilika kwa mradi huu kunatatua changamoto ya mawasiliano ya simu kwa wananchi zaidi ya laki mbili (200,000) waishio katika visiwa vya Pemba na Unguja, ambapo sasa wananchi hao wananufaika na huduma ya mawasiliano, ikiwa ni pamoja na kufanya biashara ya kuuza vocha, kufungua vibanda vya kutoa huduma za miamala ya kifedha pamoja na masuala mengine ya kijamii.

Aidha baada ya kukamilika kwa mradi huu ambao kwa kiasi kikubwa umetatua kwa kiasi kikubwa changamoto za mawasiliano katika visiwa vya Zanzibar. Hata hivyo Serikali inaendelea kufanya tathmini kuona kama bado kuna maeneo yenye changamoto za mawasiliano  ili kuyatafutia ufumbuzi kwa kadri ya upatikanaji w fedha.

Mradi huu umetekelezwa kwa ruzuku ya Serikali inayotolewa na UCSAF ambapo kiasi cha Shilingi bilioni 6.9 kilitengwa kutekeleza mradi huo.