Mradi wa kuboresha huduma ya utangazaji

  • 14 September, 2021
Mradi wa kuboresha huduma ya utangazaji

Mradi huu unalenga kusaidia radio jamii zilizopo katika mikoa mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia watanzania waliopo katika mikoa mbalimbali kupata taarifa za maeneo yao husika. Tathmini (survey) ya maeneo ya ujenzi wa minara ambayo itaendeshwa na Halmashauri za Wilaya ili mtoa huduma yeyote mwenye Redio Jamii katika eneo hilo aje afunge vifaa vyake vya utangazaji kwa gharama nafuu imekamilika.

Kupitia mradi huu, UCSAF inajenga minara husika na kuzikabidhi Halmashauri husika kwa ajili ya uendeshaji kwa sharti la kuwaruhusu wawekezaji wengine katika Wilaya kutumia mnara huo kwa gharama nafuu. Kwa kuanzia maeneo yatakayonufaika na mradi huo ni pamoja na Halmshauri ya Wilaya ya Kasulu, Ileje, Mtama, Same, Kilindi, Mbulu na Rufiji. Katika kipindi husika, zabuni ilitangazwa na kupokelewa, tathmini kufanyika na report kupelekwa katika Bodi ya Zabuni na kuidhinishwa. Mkataba wa ujenzi wa minara hiyo umetiwa saini tayari kwa ajili ya utekelezaji. Gharama za utekelezaji wa mradi huo ni shilingi bilioni 2.1.