Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF)

KONGAMANO LA C2C (CONNECT TO CONNECT)

18 September, 2024 - 19 September, 2024
08:00:00 - 14:00:00
Gran Melia Hotel, Arusha
PR - Celina ()

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ilisaini mkataba wa makubaliano na kampuni ya Extensia Limited ya Uingereza Julai 25, 2022  lengo likiwa ni kuandaa Kongamano litakalowakutanisha wadau wa sekta ya mawasiliano wa ndani na nje ya nchi linalojulikana kama Connect To Connect. Kongamano hilo pia linalenga kuzidi kukuza matumizi ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na kufungua wigo wa mifumo, ubunifu na uwekezaji katika TEHAMA. Kongamano la C2C  kwa mwaka 2024 linafanyika katika Hoteli ya Gran Meliá jijini Arusha tarehe 18 - 19 Septemba 2024.

KONGAMANO LA C2C (CONNECT TO CONNECT)
Je, una swali lolote kuhusu Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF)? Faili Maoni na Malalamiko! Universal Communications Service Access Fund Ripoti Hapa
Tuma malalamiko na mrejesho wako