WANANCHI WA MAENEO YA VIJIJINI MILIONI 2.7 KUNUFAIKA NA MRADI WA UJENZI WA MINARA 201 YA MAWASILIANO.
Wananchi wa maeneo ya vijijini nchini, wanaokadiriwa kufikia takribani milioni 2.7, wanatarajiwa kunufaika na huduma bora za mawasiliano kufuatia utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Minara ya Mawasiliano ya Simu Awamu ya Kumi (10), ambao mikataba yake imesainiwa hivi karibuni kati ya Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) na makampuni ya mawasiliano ya simu.
Kupitia mradi huo, jumla ya minara 201 itajengwa katika kata 201 zenye vijiji 263, hususan katika maeneo ya vijijini ambayo awali yalikuwa hayana au yalikuwa na huduma hafifu za mawasiliano. Ujenzi wa minara hiyo unalenga kuongeza upatikanaji wa huduma za uhakika za simu na intaneti kwa wananchi.
#UCSAF #MawasilianoKwaWote #DigitalTanzania #DigitalEconomy #DigitallyInclusiveTanzania.