Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF)

SHULE 210 ZIMEFIKISHIWA VIFAA VYA TEHAMA KUPITIA UCSAF

Imewekwa: 07 November, 2024
SHULE 210 ZIMEFIKISHIWA VIFAA VYA TEHAMA KUPITIA UCSAF

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Jerry Silaa amesema, jumla ya walimu 300 kutoka shule za Msingi na Sekondari nchini wanapatiwa mafunzo ya TEHAMA kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kufundisha na kutatua matatizo madogo madogo ya vifaa vya TEHAMA vinavyotolewa na Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) katika shule hizo.

Waziri Silaa ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo hayo katika Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam(DIT), kituo ambacho kilikuwa na walimu 100 pamoja na wengine 200 ambao wamepata mafunzo katika Chuo Kikuu cha Dodoma na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST).

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Mhandisi Peter P. Mwasalyanda amesema, hadi sasa jumla ya shule 210 zimepatiwa vifaa vya TEHAMA ikiwemo kompyuta na projekta kupitia mradi wa kuzipatia shule vifaa vya TEHAMA na kuziunganisha shule na mtandao wa intaneti.

Je, una swali lolote kuhusu Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF)? Faili Maoni na Malalamiko! Universal Communications Service Access Fund Ripoti Hapa
Tuma malalamiko na mrejesho wako