MINARA 306 KATI YA 758 IMEANZA KUTOA HUDUMA KWA WANANCHI
MINARA 306 KATI YA 758 IMEANZA KUTOA HUDUMA KWA WANANCHI
Imewekwa: 19 December, 2024
Serikali kupitia UCSAF inatekeleza mradi wa ujenzi wa minara 758 katika kata 713 ambapo jumla ya wananchi milioni 8.5 watapata huduma hiyo pindi mradi ukikamilika. Mradi huu ni wa muda wa miaka miwili ambapo unatarajiwa kukamilika ifikapo tarehe 12 Mei, 2025 na ruzuku iliyotumika katika kutekeleza mradi husika ni TZS 126 Bilioni.
Hadi kufikia Disemba 3, 2024 jumla ya minara 306 kati ya 758 ilikuwa imewaka na tayari imeanza kutoa huduma kwa wananchi.