Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF)

MINARA 332 KATI YA 758 IMEANZA KUTOA HUDUMA KWA WANANCHI

Imewekwa: 06 January, 2025
MINARA 332 KATI YA 758 IMEANZA KUTOA HUDUMA KWA WANANCHI

Serikali kupitia UCSAF inatekeleza mradi wa ujenzi wa minara 758 katika kata 713 ambapo jumla ya wananchi milioni 8.5 watapata huduma hiyo pindi mradi ukikamilika. Mradi huu ni wa muda wa miaka miwili ambapo unatarajiwa kukamilika ifikapo tarehe 12 Mei, 2025 na ruzuku iliyotumika katika kutekeleza mradi husika ni TZS 126 Bilioni.

Hadi kufikia Disemba 31, 2024 jumla ya minara 332 kati ya 758 ilikuwa imewaka na tayari imeanza kutoa huduma kwa wananchi.

Je, una swali lolote kuhusu Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF)? Faili Maoni na Malalamiko! Universal Communications Service Access Fund Ripoti Hapa
Tuma malalamiko na mrejesho wako