Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF)

MINARA 661 KATI YA 758 YAANZA KUTOA HUDUMA KWA WANANCHI.

Imewekwa: 16 August, 2025
MINARA 661 KATI YA 758 YAANZA KUTOA HUDUMA KWA WANANCHI.

Serikali ya Tanzania kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) inaendelea kutekeleza kwa mafanikio mradi wa ujenzi wa minara 758 ya mawasiliano vijijini, hii ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali kuhakikisha wananchi waishio maeneo ya vijijini wanapata huduma bora za mawasiliano ya simu na intaneti.

Hadi kufikia tarehe 15 Agosti 2025, jumla ya minara 661 kati ya hiyo 758 imekamilika na tayari imeanza kutoa huduma kwa wananchi, huku utekelezaji wa mradi huo ukiwa umefikia asilimia 87.20. Ujenzi wa minara hii ni sehemu ya mkakati wa kupunguza pengo la mawasiliano kati ya maeneo ya mijini na vijijini, na kuongeza fursa za kijamii na kiuchumi kwa wananchi wote.

Wananchi katika maeneo ambako minara imekamilika wameripoti maboresho makubwa ya huduma za mawasiliano, hali inayorahisisha shughuli za kila siku kama vile biashara, elimu kwa njia ya mtandao, huduma za kifedha, na upatikanaji wa taarifa muhimu.

Mradi huu unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na kampuni za mawasiliano nchini ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kitaifa wa kujenga uchumi wa kidijitali na kuhakikisha hakuna Mtanzania anayebaki nyuma katika zama za TEHAMA.

Je, una swali lolote kuhusu Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF)? Faili Maoni na Malalamiko! Universal Communications Service Access Fund Ripoti Hapa
Tuma malalamiko na mrejesho wako