Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF)

Mradi wa ujenzi wa Minara 758 wafikia asilimia 92.74, wananchi zaidi wafikiwa na huduma.

Imewekwa: 28 August, 2025
Mradi wa ujenzi wa Minara 758 wafikia asilimia 92.74, wananchi zaidi wafikiwa na huduma.

Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) umeendelea kusonga mbele katika utekelezaji wa mradi mkubwa wa ujenzi wa minara 758 ya mawasiliano vijijini. Hadi sasa, jumla ya minara 703 imekamilika na kuanza kutoa huduma kwa wananchi, hatua inayofanya utekelezaji wa mradi huo kufikia asilimia 92.74.

Kupitia minara hii, wananchi waishio vijijini na katika maeneo yenye changamoto za upatikanaji wa mawasiliano wameanza kunufaika kwa kupata huduma muhimu za simu na intaneti. Hatua hiyo imesaidia kuongeza fursa za kielimu, kiuchumi na kijamii pamoja na kuimarisha ushiriki wa wananchi katika maendeleo ya kidijitali.

UCSAF inaendelea na jitihada za kuhakikisha minara iliyosalia inakamilika kwa wakati, ili kufanikisha dhamira ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuhakikisha kila Mtanzania anafikiwa na huduma za mawasiliano bila kujali mahali alipo.

Mradi huu ni sehemu ya malengo ya kimkakati ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kujenga taifa lenye uchumi wa kidijitali na kupunguza pengo la mawasiliano kati ya mijini na vijijini.

Je, una swali lolote kuhusu Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF)? Faili Maoni na Malalamiko! Universal Communications Service Access Fund Ripoti Hapa
Tuma malalamiko na mrejesho wako