Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF)

WAZIRI SILAA AAGIZA SHULE YA LULUMBA KUPATIWA VIFAA VYA TEHAMA

Imewekwa: 24 October, 2024
WAZIRI SILAA AAGIZA SHULE YA LULUMBA KUPATIWA VIFAA VYA TEHAMA

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry William Silaa (Mb.), ameiagiza Wizara Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UVSAF) kuipatia vifaa vya TEHAMA pamoja na kuiunganisha na mtandao wa intaneti shule ya Sekondari Lulumba iliyoko Wilayani Iramba Mkoani Singida, kwa lengo la kuboresha mchakato wa kujifunza na ufundishaji katika shule hiyo.

Waziri Silaa ameyasema hayo wakati wa ziara yake inayoendelea katika Mkoa wa Singida, ambapo akiwa katika wilaya ya Iramba amekagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo katika shule hiyo, mradi ambayo unagharimu jumla ya shilingi milioni 134 na ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilometa 7.7 inayojengwa kwa kiwango cha lami kwa gharama ya bilioni 9.31 ili kuwaunganisha wananchi wa Mikoa ya Singida, Simiyu na Arusha.

Aidha katika ziara hiyo pia amekagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Chuo cha Ufundi (VETA) kinachojengwa katika wilaya ya Iramba mradi ambao unatarajiwa kugharimu shilingi bilioni 1.4.

#KaziInaendelea

#RaisSamiaNaMaendeleoWasikieNaWaone

#ZiarayaWaziriSilaaSingida #kaziiendelee

Je, una swali lolote kuhusu Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF)? Faili Maoni na Malalamiko! Universal Communications Service Access Fund Ripoti Hapa
Tuma malalamiko na mrejesho wako