Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF)

KAMISHNA TUME YA UTUMISHI WA UMMA AFANYA ZIARA UCSAF

Imewekwa: 14 September, 2026
KAMISHNA TUME YA UTUMISHI WA UMMA AFANYA ZIARA UCSAF

Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma, Mhe. Susan Mlawi, akiwa ameambatana na Katibu wa Tume hiyo, Bw. Nolasco Jacob Kipanda, amefanya ziara ya kikazi katika ofisi za Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), ambapo amekutana na kufanya mazungumzo na Menejimenti pamoja na watumishi wa Mfuko huo.

Ziara hiyo imelenga kujenga uelewa kuhusu usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma na kuzungumza na watumishi kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu utendaji kazi na utekelezaji wa majukumu kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mhe. Mlawi amesisitiza umuhimu wa taasisi za Serikali kuendelea kuimarisha utendaji wenye uadilifu, uwajibikaji na weledi ili kuhakikisha huduma zinazotolewa zinakuwa na tija na kuleta manufaa kwa wananchi.

Kwa upande wake Menejimenti ya UCSAF imewashukuru viongozi hao kwa ziara hiyo na kueleza kuwa ushirikiano na Tume ya Utumishi wa Umma ni muhimu katika kuimarisha utendaji na ustawi wa watumishi, pamoja na kuhakikisha Mfuko unaendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Ziara hiyo imeambatana pia na mazungumzo na watumishi wa UCSAF kuhusu masuala mbalimbali ya kiutumishi, huku viongozi hao wakipata fursa ya kusikiliza maoni na changamoto zinazowakabili watumishi katika utekelezaji wa majukumu yao

Je, una swali lolote kuhusu Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF)? Faili Maoni na Malalamiko! Universal Communications Service Access Fund Ripoti Hapa
Tuma malalamiko na mrejesho wako