UCSAF YAKAGUA MAABARA YA KOMPYUTA SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA MSALATO
UCSAF YAKAGUA MAABARA YA KOMPYUTA SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA MSALATO
Imewekwa: 23 January, 2025

Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Mhe. Balozi Valentino Longino Mlowola, imefanya ziara muhimu katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Msalato, iliyopo jijini Dodoma, kwa lengo la kukagua na kupata taarifa ya matumizi ya maabara ya kompyuta (Computer Lab) iliyojengwa na UCSAF ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa kuunganisha shule za umma na mtandao wa intaneti.
Kupitia mradi huo UCSAF huzipatia shule za umma vifaa vya TEHAMA kwa lengo la kusaidia wanafunzi katika kujifunza na kuwajengea uwezo wa kutumia vifaa hivyo ili kukabiliana na changamoto za ulimwengu wa sasa wa kidijitali.