Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF)

UCSAF YAIMARISHA USHIRIKIANO NA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA.

Imewekwa: 08 September, 2026
UCSAF YAIMARISHA USHIRIKIANO NA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA.

Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Bw. Mulembwa Munaku, akiwa ameambatana na Menejimenti ya Mfuko huo, amefanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), jijini Dar es Salaam ambapo amepokelewa na Postamasta Mkuu wa Shirika hilo, Bw. Macrice  Mbodo, pamoja na Menejimenti ya TPC.

Lengo la ziara hiyo ni kuendelea kujenga na kuimarisha mahusiano na ushirikiano kati ya UCSAF na TPC, hususan katika utekelezaji wa miradi inayotekelezwa kwa ushirikiano baina ya taasisi hizo kwa lengo la kuimarisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano kwa wananchi.

Katika ziara hiyo, viongozi na Menejimenti za taasisi hizo wamejadili maeneo mbalimbali ya ushirikiano, pamoja na namna ya kuimarisha utekelezaji wa miradi ya pamoja, ikiwemo kuwezesha huduma za Posta kufikishwa katika ngazi ya vijiji nchini kama ilivyo kwa huduma za mawasiliano ya simu, pamoja na kuendeleza Posta kidigitali kupitia matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), ili kuongeza ufanisi wa huduma za Posta na kuwafikia wananchi wengi Zaidi

Je, una swali lolote kuhusu Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF)? Faili Maoni na Malalamiko! Universal Communications Service Access Fund Ripoti Hapa
Tuma malalamiko na mrejesho wako