UCSAF yatangaza zabuni ya kufikisha mawasiliano mipakani

  • 15 September, 2021
UCSAF yatangaza zabuni ya kufikisha mawasiliano mipakani

Kwa muda mrefu kumekuwa na changamoto ya muingiliano wa mawasiliano na wananchi waishio mipakani kupata ya mawasilino ya nchi jirani hali ambayo kwa upande mmoja inawakosesha wananchi hao haki ya kupata habari na mawasiliano kutoka nchini mwao, lakini kwa upande wa pili ulinzi na usalama wa nchi unakuwa mashakani kutokana na hali hiyo.

Ili kuondoa kero hiyo na kuhakikisha maeneo yote ya mipakani yanapata mawasiliano ya ukakika pamoja na kuhakikisha usalama wa nchi katika maeneo ya mipakani, Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), imetangaza zabuni ya kufikisha huduma za mawasiliano maeneo ya mipakani na kanda maalumu awamu ya sita ambapo Kata 190 zenye Vijiji 380 zitanufaika na imetengwa sh. bilioni 26.83 kufanikisha hilo.

Zabuni nyingine inalenga kufikisha mawasiliano katika ofisi za Halmashauri za Wilaya na Kanda maalumu katika kata 34 zenye vijiji 45 huku ikitengezwa sh. bilioni 10.88 lengo likiwa ni kufikisha na kuboresha huduma za mawasiliano katika maeneo hayo

Katika kipindi cha Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Justina Mashiba, mfuko umefanikiwa kukamilisha miradi ya mawasiliano ya simu katika kata 84 zenye vijiji 305 ambapo wakazi zaidi ya 700,000 wamenufaika na mradi huo.