Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF)

WANANCHI WATAKIWA KULINDA MIUNDOMBINU YA MAWASILIANO KATIKA MAENEO YAO

Imewekwa: 16 January, 2025
WANANCHI WATAKIWA KULINDA MIUNDOMBINU YA MAWASILIANO KATIKA MAENEO YAO

Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb), amewataka wananchi wa Kata ya Itaro, wilayani Musoma Mkoani Mara kuhakikisha kuwa wanalinda na kuutumia kwa manufaa mnara wa mawasiliano ya simu uliojengwa na kampuni ya simu ya Vodacom kwa ruzuku inayotolewa na Serikali kupitia UCSAF.

Naibu Waziri Mahundi ameyasema hayo alipokuwa katika ziara ya kikazi kukagua miundombinu ya mawasiliano na upatikanaji wa huduma hiyo kwa wananchi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Amesema, Serikali imefikisha huduma hiyo muhimu kwa wananchi, ni wajibu wa wananchi kwa upande mwingine kuhakikisha kuwa wanalinda miundombinu hiyo.

Mnara huo ni miongoni mwa minara 758 inayojengwa katika kata 713 nchini, kupitia mradi wa Tanzania ya Kidijitali (DTP). Mpaka sasa jumla ya minara 349 ikiwemo mnara huo ulioko katika kata ya Itaro tayari imewaka na imeanza kutoa huduma kwa teknolojia ya 2G, 3G na 4G

Je, una swali lolote kuhusu Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF)? Faili Maoni na Malalamiko! Universal Communications Service Access Fund Ripoti Hapa
Tuma malalamiko na mrejesho wako