Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote ni nini?
Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote ulianzishwa chini ya Sheria ya Upatikanaji wa huduma ya Mawasiliano kwa Wote; Sura 422 ambayo ilikubaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo Januari 2007. Ikiwa na jukumu la Kuhamasisha ushiriki wa sekta binafsi na serikali katika utoaji wa huduma za Mawasiliano kwa Wote katika maeneo ya vijijini na maeneo ya mijini yenye Mawasiliano hafifu