MRADI WA KUONGEZA UWEZO WA MINARA YA SIMU KUPITIA UCSAF
- 26 August, 2023
Ili kuongeza matumizi ya intaneti nchini kama ilivyoainishwa katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025, UCSAF imeendelea kutekeleza mradi wa kuiongezea uwezo (upgrade) minara 126 iliyokua katika teknolojia ya 2G pekee ili iweze kutoa pia huduma ya intaneti kwa kiwango cha 3G na 4G. Minara hii ni miongoni mwa ile ambayo imejengwa kwa ruzuku iliyotolewa na Serikali kupitia UCSAF. Mpaka sasa Watoa Huduma wote wamekwisha kamilisha utekelezaji wa mradi huo ambapo jumla ya minara 126 imekwisha ongezewa nguvu. Gharama ya utekelezaji wa mradi huu ni Shilingi bilioni 3.62.