Naibu Waziri afunga mafunzo yaliyoandaliwa na UCSAF

  • 22 March, 2023
Naibu Waziri afunga mafunzo yaliyoandaliwa na UCSAF

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe, Mhandisi Kundo A. Mathew(Mb) amefunga mafunzo ya TEHAMA kwa wanafunzi wa kike wanasoma masomo ya sayansi katika shule za umma kote nchini.

Mafunzo hayo yameratibiwa na UCSAF kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dodoma( UDOM), Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya ( MUST) pamoja na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam ( DIT) ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya mtoto wa kike na TEHAMA( International Girls in ICT Day). Kwa muda wa siku tano wanafunzi wamefundishwa kutengeneza program rahisi za kompyuta ili kuwahamasisha kupenda masomo ya TEHAMA.

Baada ya mafunzo hayo,  wanafunzi wakiwa katika makundi walibuni applications za simu ambazo zitasaidia kutatua changamoto katika jamii zao.  Ambapo mbele ya Mgeni Rasmi, wanafunzi wameonyesha kwa vitendo( demostration) ya jinsi applications hizo zinavyofanya kazi.

Applications tatu zimewasilishwa; ya kwanza ikilenga kupunguza utoro mashuleni kwa mzazi kupata taarifa kupitia kwenye app, ya pili inalenga kupambana na ukatili wa kujinsia kwa kumuwezesha mhusika( anayenyanyaswa) kutoa taarifa na ya tatu ni application kuhusu lishe na maendeleo ya afya ya mtoto kuanzia kuzaliwa hadi anapofikisha miaka mitano.

Wanafunzi 31 walioshiriki katika kutengeneza applications hizo wamepatiwa zawadi ya laptops kutoka UCSAF, kila mmoja amepatiwa ya kwake kwa lengo la kuwahamasisha kuendelea kujifunza zaidi masuala ya TEHAMA.