SERIKALI KUPITIA UCSAF YAENDELEA KUBORESHA MAWASILIANO MAENEO YA MIPAKANI

  • 15 March, 2024
SERIKALI KUPITIA UCSAF YAENDELEA KUBORESHA MAWASILIANO MAENEO YA MIPAKANI

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb) leo tarehe 15 Machi, 2024 amefanya ziara ya kukagua hali ya upatikanaji wa huduma za mawasiliano katika Mkoa wa Mara.

Katika Ziara hiyo, Mhe. Nape ameongozana timu ya wataalam wa wizara pamoja na taasisi zilizo chini ya wizara hiyo ambazo ni Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Shirika la Posta Tanzania (TPC) na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

Kupitia ziara amezungumzia juhudi za Serikali katika kuboresha huduma za mawasiliano hususani maeneo ya mipakani, ambapo kwa ruzuku inayotolewa na Serikali, UCSAF imekamilisha ujenzi wa mnara katika kijiji cha Kirongwe kata ya Bukura katika Wilaya ya Rorya Mkoani Mara.

Wakati huo huo kupitia mradi wa ujenzi wa minara 758 unaotekelezwa kupitia mradi wa Tanzania ya Kidigitali (DTP), Serikali inajenga minara mingine saba katika maeneo ya mipakani yaliyo ndani ya Mkoa wa Mara.