SHULE NANE ZA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM KUPATIWA VIFAA VYA TEHAMA

  • 05 September, 2023
SHULE NANE ZA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM KUPATIWA VIFAA VYA TEHAMA

Kupitia mradi wa kuunganisha shule na mtandao wa intaneti pamoja na kuzipatia vifaa vya TEHAMA, Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) unatekeleza awamu ya pili ya mradi wa kupeleka Vifaa Maalum ya TEHAMA kwa lengo la kuwawezesha wanafunzi wenye mahitaji maalum kujifunza

Katika awamu hii, shule nane (8) zitanufaika kwa kufikishiwa vifaa mbalimbali ikiwemo Braille Machine (Nukta Nundu, Laptops, Embosser (Printa ya nukta nundu), Digital Voice Recorder, Ear mood, Projectors, Printers, Digital Camera, UPS, Recorded CD (Zenye lugha za alama), OtoAcoustic Emmission Machine (OAES), Magnifiers, Ottoscope, Ear light, Advance Audiometer Machine, Auditory Brainstem Response/ABR/BERA, Hearing Aid, Hearing Aid Batteries(Box), Braille service kit, Thermal Printer na Flash.

Shule zitakazonufaika ni pamoja na Sekondari ya Patandi maalum (Meru- Arusha), Sekondari ya Kyela (Mbeya), Sekondari ya wavulana Bwiru (Ilemela- Mwanza) na Sekondari ya Kilosa (Kilosa-Morogoro). Shule nyingine ni pamoja na, Sekondari ya Njombe Viziwi (Njombe), Sekondari ya Wasichana Rugambwa (Bukoba- Kagera), Sekondari ya Alli Mohamed Shein (Mjini Magharibi- Unguja) na Sekondari ya Jambiani (Kusini Unguja)