UCSAF kutekeleza mradi wa Tanzania ya kidijiti.

  • 04 April, 2023
UCSAF kutekeleza mradi wa Tanzania ya kidijiti.

Katika kuhakikisha kuwa watanzania wote wanapata huduma za mawasiliano nchini, Serikali kupitia UCSAF inatekeleza mradi wa kufikisha huduma za mawasiliano katika maeneo 763 ambayo hayana huduma hiyo pamoja na kuongezea nguvu(upgrade) minara iliyokuwa katika teknolojia ya 2G kuwa teknolojia ya 3G na 4G ili kuwawezesha wananchi kupata huduma ya intaneti.

Sehemu ya kwanza ya utekelezaji wa mradi huo iko katika hatua ya manunuzi, ambapo watoa huduma za mawasiliano nchini (makampuni ya simu) wameonesha nia ya kushirikiana na Serikali kupitia UCSAF. Kampuni ya mawasiliano ya Airtel imeonesha nia ya kuchukua maeneo 111, MIC ( Tigo/Zantel) maeneo 185, Vodacom maeneo 137 na TTCL maeneo 4. Mradi huu unatekelezwa na Serikali kupitia mradi wa Tanzania ya kidijiti, ambapo kiasi cha ruzuku ya shilingi bilioni 55.6 kitatolewa.

Sehemu ya pili ya utekelezaji wa mradi wa kufikisha huduma ya mawasiliano  katika kata 319 pia iko katika hatua za manunuzi  ambapo jumla ya kiasi cha shilingi bilioni 71.1 zimetegwa kama ruzuku ya kutekeleza mradi huu.