UCSAF yatoa vifaa vya TEHAMA kwa skuli ya Kizimkazi

  • 31 August, 2023
UCSAF yatoa vifaa vya TEHAMA kwa skuli ya Kizimkazi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amekagua vyumba vya madarasa vilivyokarabatiwa pamoja na chumba cha TEHAMA vilivyoko katika skuli ya Kizimkazi Mkunguni, Mkoa wa Kusini Unguja visiwani Zanzibar.

Vifaa vya TEHAMA katika chumba hicho vimenunuliwa na Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote( UCSAF), kwa kushirikiana na taasisi ya Mwanamke Initiative Foundation ( MIF).

Uzinduzi wa vyumba hivyo umefanywa na Mhe. Rais ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za kuelekea kilele cha tamasha la Kizimkazi. Katika uzinduzi huo viongozi mbalimbali wa UCSAF wamehudhuria akiwemo Mtendaji Mkuu Bi. Justina Mashiba.