UTEKELEZAJI MIRADI YA MAWASILIANO YA SIMU

  • 26 August, 2023
UTEKELEZAJI MIRADI YA MAWASILIANO YA SIMU

Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) unaendelea kutekeleza majukumu yake ya msingi kama yalivyoainishwa katika Sheria iliyoianzisha. Hadi kufikia Juni, 2023, Serikali kupitia UCSAF ilikuwa imekwishaingia makubaliano na watoa huduma kufikisha huduma za mawasiliano katika kata 1,973 zenye vijiji 5,108 vyenye wakazi 23,786,375.

Aidha, kati ya kata hizo 1,973, Miradi katika Kata 1,180 zenye vijiji 3,552 na wakazi 14,434,208 imekamilika na Watanzania waishio katika maeneo hayo wanapata huduma za mawasiliano. Utekelezaji wa ujenzi wa minara katika kata zingine 793 zenye vijiji 1,556 na wakazi 9,352,167 unaendelea na ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.

Miradi hii ya ujenzi  wa miundombinu ya mawasiliano( minara) inatekelezwa na UCSAF ambapo, ruzuku hutolewa kwa watoa huduma za mawasiliano ikiwa ni mchango wa Serikali katika ujenzi wa miundombinu hiyo na kwamba gharama zingine zote za kumalizia ujenzi wa miundombinu hiyo pamoja na gharama za uendeshaji wa miundombinu hiyo ni wajibu wa watoa huduma hao kwa kila mmoja.