WAZIRI MKUU AZINDUA REDIO ILIYOBORESHWA NA UCSAF

  • 10 January, 2024
WAZIRI MKUU AZINDUA REDIO ILIYOBORESHWA NA UCSAF

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), amezindua Kituo cha Radio Jamii Ruagwa (Ruangwa FM Redio), ambacho kimekarabatiwa na kufungwa vifaa vipya na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote(UCSAF).

Akizindua kituo hicho kilicho katika Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi, Waziri Mkuu Majaliwa amesisistiza kuwa nia ya Serikali ni kuhakikisha kuwa wananchi wote wa Tanzania wanapata habari kama ilivyoainishwa katika ibara 18 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nae, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb), ametoa wito kwa uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa na wafanyakazi wa Radio hiyo, kuhakikisha kuwa vifaa hivyo vinatunzwa ili vitumike kwa maslahi ya umma. Pia ameitaka radio Ruangwa kuandika habari za kimaendeleo kwa kuzingatia mila na desturi za kitanzania

Akitoa taarifa ya mradi, Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Justina Mashiba amesema kwa sasa redio inasikika vizuri kwenye vijiji 89 kati ya vijiji 92 vilivyo katika wilaya hiyo, huku akiongeza kuwa wananchi katika maeneo ya Masasi, Nachingwea na Kilwa wanafikiwa na mawimbi ya redio Ruangwa.

Uzinduzi wa kituo hicho ambacho maboresho yake yamegharimu zaidi ya shilingi milioni 550, ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi za Ilani ambayo inalenga kuboresha sekta ya habari kwa kuongeza wigo wa upashanaji wa habari na hivyo kuongeza wigo wa wananchi kupata habari.