Kazi za Mfuko

  1. Kubaini maeneo ya miradi ya mawasiliano ambayo yanaweza kupata ruzuku kutoka katika Mfuko;
  2. Kuweka vigezo vya utambuzi wa maeneo ya vijiji vinavyohitaji na ambavyo haviwezi kupata huduma ya mawasiliano kwa sababu havina mvuto wa kibiashara;
  3. Kuweka vigezo sahihi vya utoaji wa ruzuku kwa watoa huduma za Mawasiliano kwa ajili ya kupeleka mawasiliano katika maeneo yaliyoainishwa;
  4. Kutathmini miradi ya mawasiliano inayowasilishwa na waatoa huduma ili kupewa ruzuku na Mfuko;
  5. Kufanya tafiti mbalimbali na kufuatilia maendeleo ya mawasiliano katika maeneo ya vijijini na yale yasiyo na mvuto wa kibiashara;
  6. Kuishauri Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuhusiana na mambo yanayohusu Mawasiliano kwa wote;
  7. Kuangalia njia sahihi za kutoa ruzuku kwa ajili ya kupeleka huduma ya mawasiliano vijijini na katika maeneo yasiyo na mvuto kibiashara;
  8. Kusimamia kisheria mikataba ya utekelezaji wa majukumu ya utoaji wa huduma za mawasiliano kwa wote;
  9. Kuweka utaratibu mzuri wa kusimamia, kukokotoa na kukusanya tozo za Mawasiliano kwa wote kutoka kwa watoa huduma;
  10. Kukokotoa, kupanga na kugawanya ruzuku za mawasiliano kwa wote;
  11. Kupendekeza sera madhubuti za Mfuko kwa Waziri wa Sekta ya Mawasiliano;
  12. Kushauriana na Kushirikiana na Wizara za Serikali, Idara au Mamlaka inayojitegemea kuhusiana na masuala ya huduma kwa wote.