Wasichana na TEHAMA

  • 05 April, 2023
Wasichana na TEHAMA

Mfuko wa Mawasilano kwa Wote (UCSAF) unaendesha mafunzo ya TEHAMA kwa wanafunzi wa kike wanaosoma masomo ya sayansi ili kuwahamasisha wanafunzi hao kuchagua michepuo na fani za TEHAMA. Hii ni nafasi nzuri kwa UCSAF kukuza na kujenga uelewa wa wasichana juu ya fursa zilizopo kwenye sekta ya TEHAMA. Katika mwaka wa Fedha 2022/2023, UCSAF imetoa mafunzo kwa wasichana 248 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar. Katika miaka iliyopita UCSAF ilitoa mafunzo ya TEHAMA na uandishi wa program rahisi za kompyuta kwa wanafunzi wasichana 696 kutoka Tanzania Bara na Visiwani.