Huduma zetu

Ujenzi wa Vituo vya TEHAMA Zanzibar
  • 14 Sep, 2021
Ujenzi wa Vituo vya TEHAMA Zanzibar

Mfuko umejenga vituo 10 vya TEHAMA kwa upande wa Tanzania Visiwani. Vituo hivyo kumi 10 vimejengwa Pemba na Unguja, ambapo vituo vinne vimejengwa katika kisiwa cha Pemba na vituo sita vimejengwa katika kisiwa cha Unguja. Vituo hivyo vinatoa huduma mbalimbali ikiwemo huduma za msingi kama kudurufu nyaraka mbalimbali, kupiga simu, kutoa huduma za kutuma na kupokea fedha pamoja na kutumika kama kituo cha mafunzo ya matumizi ya vifaa vya TEHAMA.