Kupeleka na kuboresha huduma ya mawasiliano ya simu

  • 14 September, 2021
Kupeleka na kuboresha huduma ya mawasiliano ya simu

Mpaka sasa, jumla ya kata 1,197 zenye vijiji 3,613 na wakazi takribani 14,572,644 wameshafikishiwa Huduma ya Mawasiliano kwa jumla ya minara 1,321 iliyojengwa tayari katika kata hizo. Utekelezaji unaendelea katika kata 777 yenye minara 828, vijiji 1,498 na wakazi 9,226,204. Gharama (Ruzuku) za utekelezaji wa miradi hiyo ni takriban TZS bilioni 326.

Miradi hii ya mawasiliano hutekelezwa kwa ruzuku ambayo hutolewa kupitia UCSAF ikiwa ni mchango wa Serikali katika ujenzi wa miundombinu ya  huduma za mawasiliano kwa ushirikiano na watoa huduma na kwamba gharama zingine zote za kumalizia ujenzi wa miundombinu hiyo pamoja na gharama za uendeshaji wa miundombinu hiyo ni wajibu wa watoa huduma hao kwa kila mmoja.