Huduma zetu

Kuunganisha shule na mtandao wa intaneti
  • 14 Sep, 2021
Kuunganisha shule na mtandao wa intaneti

Mradi huu unalenga kuanzisha au kuboresha maabara za kompyuta katika shule za Serikali ikiwa ni pamoja na kuzipatia shule vifaa vya TEHAMA na kuziunganisha kwenye mtandao wa intaneti ili kuwapa wanafunzi nafasi ya kujifunza kutumia vifaa hivyo katika hatua za awali ili kuwajengea wanafunzi maarifa, ujuzi na ushindani. Kwa mwaka wa fedha 2020/2021 Mfuko umetekeleza mradi huu katika shule 159 nchini kote. Kwa mwaka wa fedha 2021/2022, Mfuko umepanga kutekeleza mradi huu katika shule 100.