Mafunzo ya TEHAMA kwa Walimu

  • 14 September, 2021
Mafunzo ya TEHAMA kwa Walimu

 Serikali kupitia UCSAF inaendelea kutoa mafunzo ya TEHAMA kwa Walimu 650 wa shule za umma ambazo zilinufaika na miradi ya UCSAF kwa namna moja au nyingine. Lengo la mradi huu wa mafunzo ya TEHAMA ni kusisimua matumizi ya Teknolojia hasa kwa Walimu ili wawe na ufahamu na uelewa katika taaluma ya TEHAMA ili waweze kuifundisha kwa vijana katika shule wanazotoka. Katika mafunzo hayo ya TEHAMA walimu hupata fursa mbalimbali ya kujifunza matumizi ya vifaa hivi vya TEHAMA ikiwa ni pamoja na namna ya kuvifanyia matengenezo ya msingi vifaa vya TEHAMA yaani “Basic troubleshooting skills” pindi vinapopata hitilafu ndogo ndogo.      

Mafunzo haya huendeshwa kwa kushirikiana na wadau kutoka katika vituo vitatu ambavyo ni Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Taasisi ya Teknolojia ya Dar es salaam (DIT) na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mbeya (MUST). Katika mwaka wa fedha 2022/23 na katika kipindi cha kuanzia Julai – Disemba 2022, UCSAF ilitekeleza mradi husika ambapo jumla ya Walimu 635  walipata mafunzo hayo ya TEHAMA katika vituo vya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Taasisi ya Teknlojia ya Dar es Salaam (DIT) na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mbeya (MUST).  Kati ya walimu 635 walimu 576 walitoka Tanzania Bara na walimu 59 walitoka Zanzibar.