Maombi ya kupigiwa kura katika tuzo za ITU WSIS 2024

  • 21 March, 2024

MAOMBI YA KUPIGIWA KURA KWA MRADI WA MAWASILIANO YA SIMU ULITEKELEZWA NA MFUKO WA MAWASILIANO KWA WOTE ( UCSAF), VISIWANI ZANZIBAR.

Shirika la Mawasiliano Duniani (ITU) kwa kushirikiana na Mkutano wa Dunia Wa Jumuiya ya Habari (WSIS) na waratibu wake wameandaa mkutano wa kilele wa WSIS kwa mwaka 2024, mkutano huo ni mfululizo wa mikutano inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa kwa lengo la kujadiliana kuhusu fursa na changamoto za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika karne hii.

Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) tunayo furaha kuufahamisha umma kuwa mradi wetu wa ujenzi wa minara 42 ya mawasiliano ya simu Visiwani Zanzibar umechaguliwa kuingia kwenye hatua ya kupigiwa kura. Hatua hii ni muhimu kwa kuwa inalenga kuonyesha mchango wa Tanzania katika kutumia TEHAMA katika kujiletea maendeleo.

JINSI YA KUPIGA KURA:

Click on the following URL: https://www.itu.int/net4/wsis/stocktaking/Prizes/2024

JINA LA MRADI: RURAL TELECOMMUNICATIONS IN ZANZIBAR

KIPENGELE: AL C2. INFORMATION AND COMMUNICATION INFRASTRUCTURE

NOTE: Kumbuka unaweza kupigia kura mradi mmoja tu kwenye kila kipengele

Tarehe ya mwisho ya kupiga kura  Machi 31, 2024