Matukio

Mkutano na wamiliki na wawakilishi wa vyombo vya habari Mkoani Dodoma
  • 28 Sep, 2021
  • Jakaya Kikwete Convention center Dodoma.
  • 09:00am-02:00pm
Mkutano na wamiliki na wawakilishi wa vyombo vya habari  Mkoani Dodoma

Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) unatarajia kufanya Kikao na Wamiliki au wawakilishi wa vyombo vya Habari vilivyoko Mkoani Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Posta Duniani. Mfuko unatumia fursa hii kujenga na kuimarisha mahusiano na vyombo vya Habari wakiwa ni wadau muhimu katika utekelezaji wa majukumu yake kwa njia ya kutoa elimu kwa umma.

Kikao hicho kinatarajiwa kufanyika siku ya Ijumaa, tarehe 08 Oktoba, 2021 jijini Dodoma kuanzia saa 3.00 asubuhi katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Convention center Dodoma. Mgeni Rasmi katika Kikao hicho anatarajiwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dr. Zainabu Chaula.

Ukiwa kama Mmiliki au mwakilishi wa chombo cha habari kilichoko jijini Dodoma unaalikwa wewe au mwakilishi wako mmoja tu kuhudhuria Kikao hicho. Kwa maelezo zaidi wasiliana na Bi. Celina Mwakabwale kupitia barua pepe ya celina.mwakabwale@ucsaf.go.tz