Waziri Nape azindua mnara uliofadhiliwa na UCSAF Mkoani Njombe

  • 10 January, 2023
Waziri Nape azindua mnara uliofadhiliwa na UCSAF Mkoani Njombe

 

Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe.Nape Moses Nnauye (Mb),amezindua mnara wa mawasiliano ya simu uliojengwa na Kampuni ya simu ya Vodacom kupitia ruzuku inayotolewa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote(UCSAF).Mnara huo umejengwa katika kijijiji cha Kinenulo kata ya Imalinyi wilaya ya Wanging’ombe mkoa wa Njombe. 

Katika uzinduzi huo Mhe,Nnauye ameipongeza UCSAF kwa kazi nzuri ya kufikisha huduma za mawasiliano kwa wananchi waishio vijijini,huku akiitaka kuongeza juhudi katika kufikisha huduma za Mawasiliano kwa wananchi popote walipo bila kujali maeneo yao.

Katika uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa wa Njombe Bw. Anthony Mtaka ameishukuru na kuipongeza UCSAF kwa kutatua changamoto ya mawasiliano katika kijiji cha Kinenulo,na kutoa rai kwa wananchi kutunza miundombinu ya mnara huo.

Naye Mtendaji Mkuu wa UCSAF Bi.Justina Mashiba amesema mnara huo umejengwa kwa uwezo wa kutoa huduma ya 2G, 3G na 4G na utahudumia wananchi wapatao 8,529.

Kuwashwa kwa mnara huo kunatatua changamoto ya mawasiliano ambayo imekuwa ikiwakabili wananchi wa eneo hilo na pia utawezesha shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo biashara.