Waziri Nnauye azindua Wi-Fi iliyowezeshwa na UCSAF

  • 08 July, 2023
Waziri Nnauye azindua Wi-Fi iliyowezeshwa na UCSAF

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye amezindua huduma ya Intaneti ya Wazi (Free-Wifi) katika maeneo 17 ndani ya Viwanja vya Maonesho Sabasaba, leo tarehe 8 Julai, 2023, ikiwa ni siku ya TEHAMA katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (Sabasaba).

Huduma hiyo ya Intaneti ya wazi imewezeshwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwa kushirikiana na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kwa lengo la kuwawezesha wananchi wanaofanya biashara na wanaotembelea viwanja hivyo kupata huduma bora ya mtandao wa intaneti.