Tiba Mtandao
- 14 September, 2021
Mradi huu unalenga kuwawezeza wananchi waishio vijijini au pembezoni mwa nchi ambako hakuna huduma za madaktari bingwa kupata huduma hizo kwa njia ya mtandao bila kusafiri umbali mrefu. Ikiwa ni mwendelezo wa kuziunganisha hospitali zetu za Mikoa na rufaa na ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI), UCSAF imepanga kuziunganisha Hospitali za Rufaa za Mnazi Mmoja iliyopo Unguja na Hospitali ya Rufaa ya Abdalla Mzee iliyopo Pemba.
Katika kipindi cha Julai – Disemba, 2022, vifaa vya TEHAMA vilifungwa katika hosipitali zote pamoja na Mfumo wa Tiba Mtandao. Kwa sasa wataalamu wanaendelea na kuunganisha mfumo wa kusafirisha picha (PACS) pamoja na kuziunganisha machine za X-ray. Mradi huu unatarajia kukamilika ifikapo mwisho wa mwezi Januari 2023.